Sungura
walikuwa wakionewa sana na wanyama wengine kwa kupigwa, kuwindwa na
kuliwa, kiasi kwamba hawakujua wakimbilie wapi. Ikawa wanaishi maisha
ya karaha mno na kila walipomwona mnyama yeyote akiwakaribia,
walilazimika kutimua mbio kwa woga.
Siku moja
wakaliona kundi la Farasi pori walio katika hali ya taharuki
wakikimbia na kuwaelekea wao. Walihamaki na kutimka kuelekea ziwani,
wakiwa na nia ya kujitupa majini ili wafe, kwani waliona ni heri kufa
kuliko kuendelea kuishi katika adha na karaha ile ya kunyanyaswa, na
maisha ya roho mkononi.
Lakini
walipokaribia kingo za ziwa, kundi la Chura waliokuwa wamejipumzisha
wakitafakari, walishtushwa sana na vishindo vya Sungura hao, nao
walitaharuki wakageuka kwa woga na kujitupa ziwani kuokoa maisha yao.
“Kwa kweli,” alisema mmoja wa Sungura, “kumbe hali
yetu sisi siyo mbaya sana kama tunavyodhani.”
Nimeipenda Sana Hadithi hii napia inafuraisha.
JibuFutamavi wewe
Futavizuri sana nitalisoma
JibuFuta