Hapo zamani
kulikuwa na Kijana mmoja mtukutu ambaye alipenda sana kuchezea mimea
na wadudu. Siku moja akiwa kwenye kichaka jirani na nyumbani kwake,
aligusa Upupu kwa mkono wake wa kuume, nao ukaanza kumwasha.
Ukamletea karaha na maumivu makali.
Akaamua
kukimbilia nyumbani kwake haraka huku akiendelea kujikuna na machozi
yakimlengalenga. Alimfuata Mama yake bustanini na kumwambia kwa sauti
ya kudeka akisema,
“Mama,
Ingawa upupu unanichomachoma na kuniletea maumivu makali kiasi hiki,
mie niliugusa taratibu na kwa unyenyekevu. Sijui ni kwa nini
unaniumiza hivi”
“Kuugusa taratibu ndiyo haswa sababu iliyopelekea
ukuchome, na kukuumiza.” Mama yake alimwambia. “Siku nyingine
mwanangu, ukitaka kuugusa Upupu, ukamate na uufinye kwa nguvu, nao
utakuwa laini na mororo kiganjani mwako, na wala hautokuchoma na
kukuumiza hata kidogo.”
Hadithi hii
inatufundisha nini?
1……………………………………………………………………………………………………………………
2……………………………………………………………………………………………………………………
3……………………………………………………………………………………………………………………
Taja methali, nahau au
msemo wa Kiswahili wenye maana inayofanana na maudhui ya hadithi
hii;
………………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………………
0 maoni:
Chapisha Maoni