Hapo zamani
kulikuwako Mfalme, ambaye alikuwa na mtoto mmoja tu wa kiume, kijana
aliyependa sana mazoezi ya sanaa za mapigano. Kila siku
alijichanganya na vijana wa rika lake katika mazoezi na michezo. Na
awapo nyumbani alipendwa sana na wazazi wake, hasa baba yake.
Siku moja
Mfalme akiwa usingizini aliota ndoto. Na katika ndoto hiyo alipewa
onyo la kuwa mwanaye huyo wa pekee atakufa kwa kuuawa na kuliwa na
Simba.
Aliposhtuka
alipatwa na hofu, kwani katika himaya yake wanyama wakali kama Simba
kushambulia binadamu au mifugo ilikuwa kawaida.
Kwa kuhofia
huenda ndoto yake ikawa ni ujumbe wa kweli, aliamua kumjengea yule
mwanaye, Mwanamfalme, kasri kubwa maridadi.
Jengo
lilinakshiwa maridadi na kuta zote zilipambwa kwa picha nzuri za
wanyama mbalimbali, zikiwa na ukubwa unaolingana na wa wanyama
halisi. Mojawapo kati ya zile picha za ukutani ilikuwa ni picha ya
Simba dume.
Hivyo
Mwanamfalme aliwekwa ndani ya kasri, akapewa mahitaji yote humo,
akafungiwa asitoke nje hata mara moja kwa hofu ya kuuawa na Simba.
Siku moja
yule kijana mwana wa mfalme aliiona ile picha ya Simba, ndipo huzuni
yake ya kukosa uhuru na kufungiwa ikafufuka upya, na akiwa amesimama
kando ya ile picha ya Simba, aliitazama kwa jazba na kusema: “ee
mnyama ninayekuchukia kuliko wanyama wote! Kutokana na ndoto ya
uwongo aliyoota baba yangu, na kuona maono ya usingizini, nimefungiwa
ndani ya kasri hili kama mtoto wa kike, nisitoke kwa kukuhofia wewe:
nikutende nini sasa baradhuli mkubwa wee?” Akisema hivyo
aliunyoosha mkono wake wa kuume kuelekea mti wa miiba, kwa nia ya
kukata tawi atengeneze fimbo ili amsulubu yule Simba kwa kisasi.
Bahati mbaya miba moja ilimchoma kidoleni, akatokwa damu
nyingi na kupata maumivu makali sana, kiasi kwamba Mwanamfalme
alianguka chini na kuzirai. Ghafla alishikwa na homa kali, ambayo
ilimuua siku chache baadaye.
Hadithi hii
inatufundisha nini?
1……………………………………………………………………………………………………………………
2……………………………………………………………………………………………………………………
3……………………………………………………………………………………………………………………
Taja methali, nahau au
msemo wa Kiswahili wenye maana inayofanana na maudhui ya hadithi
hii;
………………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………………
0 maoni:
Chapisha Maoni