Kulitokea
usiku mmoja wa mbalamwezi Mbweha alikuwa akizungukazunguka kwa
mawindo kwenye shamba la Mkulima mwenye mifugo, ambapo aliliona
Jimbi moja limesimama juu kabisa asipoweza kufikia likiwika kwa sauti
ya juu.
“Habari
njema, habari njema!” Mbweha alipaza sauti kwa hila.
“Nijuze, ni
ipi habari hiyo njema?” Jimbi lilijibu.
“Mfalme
Simba ametoa tamko la makubaliano ya amani kwa wanyama wa ulimwengu
mzima. Kuanzia sasa ni marufuku kwa mnyama yeyote kumdhuru mwingine,
bali sote hatuna budi kuishi pamoja kwa amani na urafiki kama ndugu.”
“Shime,
hakika hiyo ni habari njema,” lilisema Jimbi; kisha likaendelea “na
kule kwa mbali namwona kuna rafiki anakuja, ambaye tunaweza kufurahi
naye pamoja, tukianza ukurasa huu mpya wa amani.” Akisema hayo
Jimbi aliinyoosha shingo yake akitazama mbali upande ule alio yule
mbweha.
“Unamwona
nani anakuja?” Mbweha aliuliza kwa hamaki.
“Ni Mbwa wa
bwana wangu ndiye anayekuja kuelekea upande wetu… Vipi, mbona
unaondoka mapema?” aliuliza, kwani Mbweha alishageuka na kuanza
kuondoka mara baada ya kusikia habari ya ujio wa Mbwa.
“Huwezi
kusubiri kidogo umpongeze Mbwa kwa kupata utawala wa sheria hii mpya
ya amani ya ulimwengu?” alimuuliza huku akitabasamu.
“Ningeliweza kufanya hivyo,” alijibu Mbweha, “ila
nahofia huenda Mbwa akawa hajasikia bado tangazo la mfalme Simba.”
Hadithi hii
inatufundisha nini?
1……………………………………………………………………………………………………………………
2……………………………………………………………………………………………………………………
3……………………………………………………………………………………………………………………
Taja methali, nahau au
msemo wa Kiswahili wenye maana inayofanana na maudhui ya hadithi
hii;
………………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………………
0 maoni:
Chapisha Maoni