Hapo zamani
za kale Sungura walianzisha vita na Tai. Mapambano yalianza na kila
upande ukijigamba na kudhani ulikuwa na uwezo wa kumshinda mwenzie.
Vita
vilipopamba moto, Sungura walihisi kuzidiwa. Baada ya vikao na
mashauriano ya majemedari, walikubaliana kutuma maombi kwa Mbweha
ili waje kama mamluki kuwasaidia kupambana na jeshi shupavu la Tai.
Mbweha wakajibu, “tungeweza kuja kuwasaidia kwa moyo
mmoja, iwapo tusingeliwafahamu ninyi ni nani, na ni nani hao
mnaopigana nao vita.”
Hadithi hii
inatufundisha nini?
1……………………………………………………………………………………………………………………
2……………………………………………………………………………………………………………………
3……………………………………………………………………………………………………………………
Taja methali, nahau au
msemo wa Kiswahili wenye maana inayofanana na maudhui ya hadithi
hii;
………………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………………
0 maoni:
Chapisha Maoni