"Ah, binamu," alisema mbwa "nilijua tu yatakukuta haya; kwamba maisha yako ya kutangatanga na yasiyo na uhakika ipo siku yatakuangamiza. Kwanini usifanye kazi maalum na ya uhakika kama nifanyavyo mimi, ili upate chakula kila mara kama nipatavyo mimi?"
"Nakubaliana na wewe kabisa ndugu yangu," alijibu Mbwa-mwitu, "endapo tu nikipata nafasi."
"Nafasi sio tatizo, mi ntakufanyia mpango," alisema Mbwa; "twende nami nyumbani kwa bwana wangu na nitamwomba akuajiri tufanye kazi pamoja nami."
Basi Mbwa-mwitu na Mbwa wakaongozana kuelekea mjini. Wakiwa bado njiani, wanakaribia kufika Mbwa-mwitu akagundua kwamba nywele kwenye sehemu fulani ya shingoni ya Mbwa zimenyonyoka na kubaki chache, hivyo akamuuliza Mbwa kulikoni.
"Oh, wala si kitu," Mbwa alijibu. "Hii ni sehemu ambayo mkanda wa nyororo hufungwa nyakati za usiku ili kunifanya nibaki sehemu moja; unauma na kukera kidogo, ila baada ya muda unazoea."
"Ha ndiyo hivyo?" alisema mbwa mwitu. "Basi kwaheri ndugu yangu, Bwana Mbwa."
***
0 maoni:
Chapisha Maoni