Siku moja
mfalme Simba akiwa amejipumzisha kivulini, alipitiwa na usingizi.
Panya mtukutu alimsogelea na kuanza kuchezacheza juu yake; hali
ambayo ilimfanya aamke mara moja. Alipoamka, Simba alimkamata Panya kwa
kumkandamiza na guu lake kubwa, tayari kwa kumla.
“Naomba
unisamehe, ee Mfalme,” Panya alilia na kuomba: “nisamehe kwa sasa
na sitosahau kamwe: huwezi kujua pengine ipo siku mimi pia ninaweza
kulipa wema wako kwa kukusaidia!.”
Simba
aliguswa sana na maneno ya Panya kwamba eti huenda ipo siku
akamsaidia yeye Simba, mnyama mkubwa ambaye ni mfalme wa wanyama
wote. Aliinua mguu wake na kumwacha aende zake.
Siku moja
Simba alinaswa kwenye mtego wa Binadamu, na wawindaji walipomkuta
walipanga kumpeleka kwa Mfalme wao kama zawadi akiwa hai vilevile.
Walimfunga kwenye mti kwa kamba kisha wakaondoka kwenda kutafuta
usafiri wa kumbebea.
Punde
ikatokea yule Panya alipita maeneo yale, na alipomwona Simba yupo
katika hali ile ya taharuki, majonzi na hofu ya kuuawa, alienda pale
mtini na kuzikatakata kwa meno yake makali kamba zile zilizomfunga
Mfalme wa wanyama wote.
“Si nilikwambia,? unaona sasa…” alisema Panya.
Hadithi hii
inatufundisha nini?
1……………………………………………………………………………………………………………………
2……………………………………………………………………………………………………………………
3……………………………………………………………………………………………………………………
Taja methali, nahau au
msemo wa Kiswahili wenye maana inayofanana na maudhui ya hadithi
hii;
………………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………………
0 maoni:
Chapisha Maoni