Mbweha
alikuwa akijigamba mbele ya Paka kuwa yeye ana mbinu nyingi sana za
kuwakwepa maadui zake.
“Nina fuko
zima la mbinu na ujanja,” alisema, “ambalo lina mamia ya njia za
kujiepusha na maadui zangu wakati wa hatari.”
“Mimi
ninayo mbinu moja tu,” alisema Paka; “lakini ninaiamini, na
inanifaa hiyo hiyo.”
Wakiongea
maneno hayo, punde wakasikia sauti za Mbwa wawindaji zikielekea
upande wao, na Paka alichupa akauparamia mti haraka na kujificha juu
kwenye matawi. “Hii ndiyo mbinu yangu,” alisema Paka. “Je
mwenzangu wafanyaje?”
Mbweha
akafikiri kwanza kutumia njia hii, mara njia ile, na kabla hajafanya
maamuzi, Mbwa walimkaribia na kumkaribia, na mwishowe Mbweha akiwa
katika mkanganyiko huo, alikamatwa na kuuawa na Wawindaji.
Paka ambaye
alikuwa akishuhudia kinachotokea, alisema;
“Heri njia moja salama kuliko njia mia ambazo huwezi
kuzitumia.”
Hadithi hii
inatufundisha nini?
1……………………………………………………………………………………………………………………
2……………………………………………………………………………………………………………………
3……………………………………………………………………………………………………………………
Taja methali, nahau au
msemo wa Kiswahili wenye maana inayofanana na maudhui ya hadithi
hii;
………………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………………
0 maoni:
Chapisha Maoni