Nguruwe mmoja
mdogo alikuwa amefungiwa kwenye uzio wa miti. Mbuzi na Kondoo pia
walifungwa pamoja naye. Siku moja Mchungaji wao alikuja na kumkamata
yule Nguruwe, ambaye aliguna na kuanza kupiga kelele na kufurukuta.
Mbuzi na
Kondoo walimlalamikia Nguruwe kwa kelele zake za kilio na
purukushani, wakasema kwa kejeli, “Mara kwa mara Mchungaji wetu
hutushika sisi, na hatuangui kilio kama yeye.”
Kusikia hivyo, Nguruwe akawajibu, “Mchungaji
anavyowashika ninyi na anavyonishika mimi ni vitu viwili tofauti
kabisa. Kwani anapowashika ninyi huhitaji kutoka kwenu sufu na maziwa
tu, lakini anaponishika mimi ana nia ya kunipokonya uhai wangu.”
Hadithi hii
inatufundisha nini?
Taja methali, nahau au
msemo wa Kiswahili wenye maana inayofanana na maudhui ya hadithi
hii;
0 maoni:
Chapisha Maoni