Mtu mmoja
alikwenda kichakani huku akiwa na shoka mikononi kwake, na kuiomba
Miti kwa unyenyekevu ili iweze kumpa tawi moja tu dogo ambalo
alisema alikuwa na kazi nalo fulani.
Miti ile
ilikuwa na tabia njema, ikampa moja ya matawi yake. Kumbe yule mtu
alikuwa akihitaji mpini wa shoka lake. Kwa kutumia tawi lile
alilopewa akakarabati shoka lake na kisha kuanza kazi ya kuikata Miti
ile mmoja baada ya mwingine.
Ndipo Miti ilipon’gamua ilitenda ujinga kwa kiasi
gani kutokana na kitendo kile cha kumsaidia adui yao mpini, ambao
ulitumika kulitengeneza shoka, ambalo lilitumika kuiangamiza Miti
yenyewe.
Hadithi hii
inatufundisha nini?
1……………………………………………………………………………………………………………………
2……………………………………………………………………………………………………………………
3……………………………………………………………………………………………………………………
Taja methali, nahau au
msemo wa Kiswahili wenye maana inayofanana na maudhui ya hadithi
hii;
………………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………………
0 maoni:
Chapisha Maoni