Siku moja
Simba alitangaza kuwa yu mgonjwa mahtuti na kwamba alikaribia kufa.
Hivyo alitoa tamko la kuwaalika Wanyama wote waende nyumbani kwake
kumwona na kusikia wosia wake wa mwisho na ushuhuda wa mambo kadha wa
kadha, na pia wapate busara za mfalme.
Hivyo Mbuzi
alienda kwenye pango alililoishi Mfalme Simba ili kumjulia hali.
Alisimama kwenye sehemu ya kuingilia pangoni na kusikiliza kwa muda
mrefu. Kisha kondoo alikuja na akaingia pangoni moja kwa moja, na
kabla hajatoka Mwanafarasi naye alikuja kupokea wosia wa mwisho wa
Mfalme, akaingia pangoni.
Baada ya muda
mfupi Simba alijitokeza nje akionekana kupata nafuu ya haraka, akaja
kwenye lango lake la kuingilia pangoni ili apunge upepo wa nje.
Alipopiga macho kushoto na kulia alimwona Mbweha, akiwa amejiinamia
anasubiri nje ya pango kwa muda mrefu.
“Kwa nini
ewe Mbweha hujaja ndani ya pango kutoa heshima zako za mwisho
kwangu? Na badala yake unakaa tu hapa nje kwa kejeli?” Simba
alimuuliza.
“Nisamehe Bwana mkubwa,” Mbweha alijitetea, “ila
katika kuja kwangu hapa nimegundua alama za nyayo za wanyama wengi
ambao wamekwisha kukutembelea pangoni mwako; na nikichunguza kwa
makini zaidi naona alama nyingi za kwato zikiingia ndani, na sioni
zitokazo nje. Hadi hapo nitakapowaona wanyama waliokwishaingia
pangoni mwako wakitoka nje, sitoingia, naona ni heri nibaki hukuhuku
nje kwenye uwazi na hewa safi.”
Hadithi hii
inatufundisha nini?
1……………………………………………………………………………………………………………………
2……………………………………………………………………………………………………………………
3……………………………………………………………………………………………………………………
Taja methali, nahau au
msemo wa Kiswahili wenye maana inayofanana na maudhui ya hadithi
hii;
………………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………………
Kwel Simba Alikuwa Anajfanya Kumbe Njaa Tupu
JibuFuta