Ilisemekana
wakati fulani kuwa Nyani mmoja alikuwa akizaa watoto wawili mapacha
katika kila mzao wake. Na alikuwa na kasumba ya kumpenda na kumjali
sana mtoto mmoja, yule mdogo, huku akimchukia na kutomjali kabisa yule
mkubwa.
Ikatokea katika mzao wake mmoja kwamba yule mdogo
aliyempenda na kumjali akasongwasongwa na kudhoofika kiafya na
kimaadili kutokana na upendo wa mamaye uliopita kiasi, wakati yule mkubwa
aliyechukiwa alipata mafundisho na kustawi licha ya kuishi maisha ya
kutojaliwa na kuchukiwa na mama yake.
Hadithi hii
inatufundisha nini?
1……………………………………………………………………………………………………………………
2……………………………………………………………………………………………………………………
3……………………………………………………………………………………………………………………
Taja methali, nahau au
msemo wa Kiswahili wenye maana inayofanana na maudhui ya hadithi
hii;
………………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………………
0 maoni:
Chapisha Maoni