Hapo zamani
za kale kulikuwako Chura mkubwa.
Siku moja
Chura huyo alijitokeza toka nyumbani kwake Kidimbwini Maguguni na
kuwatangazia wanyama wote kwa kujitapa kwamba yeye ni mtabibu mjuzi,
na ni mbobevu katika masuala ya tiba na dawa. Akatembea kifua mbele
na kujigamba kuwa ana uwezo wa kutibu magonjwa ya aina zote, kwa
jamii zote za wanyama!
Mbweha alijitokeza na kumuuliza, “Unathubutu vipi
kujifanya tabibu wa wengine, ilhali unashindwa kujitibu mwenyewe
ulemavu wako wa mwendo na makunyanzi ya ngozi!?”
Hadithi
hii inatufundisha nini?
1……………………………………………………………………………………………………………………
2……………………………………………………………………………………………………………………
3…………………………………………………………
Taja
methali, nahau au msemo wa Kiswahili wenye maana inayofanana na
maudhui ya hadithi hii;
………………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………………
0 maoni:
Chapisha Maoni