Hapo zamani
za kale kulikuwako mkutano mkuu wa wanyama kila baada ya miaka
mitatu, ambapo wanyama wote walipata fursa ya kutoa michango ya
mawazo ili kuboresha kanuni na namna ya maisha yao kama jamii moja.
Siku moja,
wakiwa katika mkutano kama huo, Sungura walitoa mawaidha kwa hisia
kali sana, rai yao ikiwa ni kutaka wanyama wote wawe na haki sawa.
“Tunataka
haki sawa kwa wanyama wote, wakubwa kwa wadogo, wala nyama kwa wala
nyasi…”
Simba ambaye alikuwa ndiye mwenyekiti wa mkutano
akawajibu: “maneno yenu, enyi Sungura! ni mazuri sana; ila hayana
makucha wala meno kama tuliyonayo sisi.”
Hadithi hii
inatufundisha nini?
1……………………………………………………………………………………………………………………
2……………………………………………………………………………………………………………………
3……………………………………………………………………………………………………………………
Taja methali, nahau au
msemo wa Kiswahili wenye maana inayofanana na maudhui ya hadithi
hii;
………………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………………
0 maoni:
Chapisha Maoni