Hapo zamani
za kale, Mwanafalsafa mmoja alikuwa na kawaida ya kwenda ufukweni mwa
bahari kila siku nyakati za jioni, kujipumzisha na kutafakari.
Ikatokea alasiri ya jumamosi moja, akiwa ufukweni kama ilivyo ada
yake, alishuhudia kwa macho yake mashua ikipigwa na dhoruba kali
na kuzama.
Mabaharia na abiria wote waliokuwamo chomboni walizama na
kufa maji.
Yule bwana alihuzunika sana, hata alifikia kulaani
kwamba majaaliwa ya Mungu hayakuwa ya haki kwani kutokana na mtu
mmoja tu ambaye alipaswa kufikwa na mauti siku ile, umati mkubwa
uliangamizwa pamoja naye. “Iweje roho za watu wote wale ziangamizwe
kwa ajili ya mtu mmoja tu ambaye alipaswa kufa leo?” alijiuliza
akiinua mikono yake juu kama ishara ya lawama kwa Mungu.
Wakati
akiendelea kutafakari mawazo yake hayo, mara akajikuta amezungukwa na
jeshi zima la Mchwa, ambao kumbe alikuwa amesimama kando ya nyumba
yao.
Mmojawapo
kati ya mchwa waliompanda miguuni alimng’ata na kumsababishia
maumivu makali sana.
Yule bwana
alighadhibika na kuanza kuwapondaponda kwa miguu na kuwaua mchwa
wote waliokuwapo karibu naye.
Mara Mekyuri alitokea, akamcharaza fimbo za maonyo yule
Mwanafalsafa huku akisema, “uu nani wewe hata ukatoa hukumu juu ya
matendo ya Mungu juu ya wanadamu, ilhali wewe mwenyewe unatenda
vivyo hivyo kwa Mchwa?”
Hadithi hii
inatufundisha nini?
1……………………………………………………………………………………………………………………
2……………………………………………………………………………………………………………………
3……………………………………………………………………………………………………………………
Taja methali, nahau au
msemo wa Kiswahili wenye maana inayofanana na maudhui ya hadithi
hii;
………………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………………
0 maoni:
Chapisha Maoni