Ng’ombe
Maksai alikwenda kunywa maji katika dimbwi ambalo lilikuwa na watoto
wa chura. Watoto hao walizaliwa hapo na kwao hiyo ilikuwa ni maskani
yao halali. Ila kwa wakati ule mama yao alikuwa ametoka, kaenda
kuitembelea familia ya rafiki yake iliyokuwa na makazi kwenye dimbwi
jingine upande wa pili wa kichaka.
Kwa bahati
mbaya, Maksai alimkanyaga mtoto mmoja wa Chura na kumjeruhi vibaya,
akafa. Punde mama yao akarejea toka matembezini na kubaini kuwa mmoja
wa watoto wake hayupo dimbwini. Akawauliza wale nduguze kulikoni.
“Mwenzetu
amekufa, mama mpenzi;” alijibu mmoja wao kwa majonzi.
“Kumetokea
nini tena mbona niliwaacha wote wazima?” mama Chura alihoji.
“Muda si
mrefu uliopita mnyama mkubwa sana alikuja dimbwini akamkanyaga kwa
kwato zake kubwa na kumuua.” walimjibu.
Chura
alihamaki mno, akaanza kuvuta pumzi na kujitunisha kwa hasira,
akahoji, “iwapo baradhuli huyo alikuwa mkubwa kiasi hicho kwa
umbo,”
“Ee mama yetu mpendwa, acha kujijaza upepo na
kujitunisha” mtoto wake mmoja alimkatisha, “na wala usighadhibike
kiasi hicho; kwani hakika nakuambia, utaanza kupasuka mwili kabla
hujafanikiwa kuiga ukubwa wa dhalimu yule.”
Hadithi hii
inatufundisha nini?
1……………………………………………………………………………………………………………………
2……………………………………………………………………………………………………………………
3……………………………………………………………………………………………………………………
Taja methali, nahau au
msemo wa Kiswahili wenye maana inayofanana na maudhui ya hadithi
hii;
………………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………………
Very nice, have reminded me my child hood
JibuFutaNimeipenda
JibuFuta