Kulikuwa na
mtu mmoja fukara sana, kazi yake ni fundi Seremala. Ndani ya nyumba
yake pamoja na vitu vingine, aliweka sanamu ya Mekyuri ambaye
aliaminika kuwa ni mjumbe wa Mungu.
Kila siku fukara huyo aliitolea
sanamu ile sadaka, na kuiomba imbariki na kumfanya kuwa tajiri.
Lakini fundi alizidi tu kuwa fukara siku hadi siku, zaidi na zaidi.
Mwishowe
alighadhibika, akaamua kuishusha sanamu ile toka kwenye kiweko chake
na kuibamiza ukutani kwa jazba.
Baada ya kichwa cha Sanamu hilo kung’oka, zikamiminika
dhahabu chungu nzima, ambazo fundi Seremala alizizoa na kusema,
“Ewaa, nadhani sanaa yako kwa ujumla ni ya mkanganyiko na
isiyoeleweka; kwani nilipokupa heshima na kukunyenyekea sikupata
mali kutoka kwako: ila sasa nimekutenda vibaya umenijazia dhahabu na
utajiri tele.”
Hadithi hii
inatufundisha nini?
1……………………………………………………………………………………………………………………
2……………………………………………………………………………………………………………………
3……………………………………………………………………………………………………………………
Taja methali, nahau au
msemo wa Kiswahili wenye maana inayofanana na maudhui ya hadithi
hii;
………………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………………
0 maoni:
Chapisha Maoni