Hapo zamani
za kale kulitokea mgogoro mkubwa sana kati ya Ndege na Wanyama, na
vita kati yao ilinukia. Ilionekana kana kwamba juhudi zote za
mapatano ziligonga mwamba. Wakati majeshi hayo mawili yakijikusanya
kujiandaa kwa mapigano ya umwagaji damu, Popo alisita kuchagua upande
wa kujiunga nao kivita.
Jeshi la
Ndege lilipita karibu na kitulio chake na kumwambia; “Twende nasi
vitani ee Popo ndege mwenzetu.”
Popo alikataa
na kusema, “Mimi ni mnyama. Wala si ndege kama ninyi”
Baadaye jeshi
la Wanyama nalo lilipita chini ya kitulio chake, walipomwona
walimwita na kumwambia; “Twende nasi vitani ee Popo myama
mwenzetu.” Popo alikataa tena na kujibu, “Mimi ni Ndege. Wala si
mnyama kama ninyi.”
Basi kukawa
na ngurumo za kutisha za wanyama shupavu kama vile simba duma na
tembo; na ndege shupavu kama tai na furukombe. Anga lote lilijaa
vitisho na harufu ya damu. Majike wenye ndama na majike wenye makinda
walihisi kiyama chao kimefika.
Kwa bahati
sana, katika dakika za mwisho mwisho kuelekea vita, muafaka ulifikiwa
kati ya pande mbili hizo na vita vikaepukwa. Kukawa na amani badala
ya mapigano. Kuona hivyo, Popo naye alitamani kuwa sehemu ya
shamrashamra hizo. Alikwenda kwa Ndege akitaka kujiunga nao katika
furaha na cherekochereko za kushangilia amani, wakamfukuza.
Akaamua
kuondoka akaenda kwa wanyama huku akitabasamu na kutegemea kushiriki
nao furaha ile ya amani. Nao walimfukuza kwa hasira hata akalazimika
kukimbia wasije wakamdhuru kwa kumjeruhi au kumtoa roho kabisa.
“Ah,” Popo alijisemea kimoyomoyo, “sasa
nimeng’amua,”
Hadithi hii
inatufundisha nini?
1……………………………………………………………………………………………………………………
2……………………………………………………………………………………………………………………
3……………………………………………………………………………………………………………………
Taja methali, nahau au
msemo wa Kiswahili wenye maana inayofanana na maudhui ya hadithi
hii;
………………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………………
0 maoni:
Chapisha Maoni