Ayala, baada
ya kukimbizwa na kuandamwa na wawindaji toka mbali, alichoka sana na
kujua sasa mwisho wake umefika. Wawindaji walipomkaribia alifanya
hila, akachupa kuume na kujibanza kwenye mvungu wa majani makubwa ya
Mzabibu.
Wawindani nao kwa haraka waliyokuwa nayo (na hulka ya kuwahi ni
kupata) hawakuweza kuing’amua hila yake, wakampita palepale bila
kumwona.
Baada ya
muda mfupi, kwa kudhani kuwa hatari haipo tena, Ayala aliinuka na
kuanza kuyanyofoa nyofoa yale majani ya Mzabibu. Mwindaji mmoja
aliyekuwa nyuma ya wenzake alisikia kwa mbali ule mchakato wa majani,
akageuka kuangalia nyuma walikotoka, akamwona yule Ayala chini ya
Mzabibu. Akachomoa mshale, akauweka kwenye upinde, akapiga na
kumchoma Ayala tumboni.
Ayala, wakati akitapatapa karibia kukata roho, alikoroma
na kusema; “Nimepata tijara nistahiliyo, kwani sikupaswa kabisa
kuyatendea vile majani ya Mzabibu ambao punde uliokoa maisha yangu.”
0 maoni:
Chapisha Maoni