Majogoo
wawili walioishi kwenye zizi moja walianza kupigana wakigombea ukuu
katika himaya yao. Mwishowe jogoo Mwekundu alimshinda jogoo Mweupe,
ambaye alisalimu amri na kukimbia.
Jogoo Mweupe
alienda kujificha kwenye kona ya mbali kwa unyonge, ilhali yule
Mwekundu aliyeshinda alirukia juu ya ukuta, akapiga mbawa zake na
kuwika kwa sauti kuu kama ishara ya kuwa yeye ndiye mkuu hakuna
mwingine zaidi yake. Ghafla Mwewe aliyekuwa akipita juu alimwona
akamkamata na kumbeba kwa makucha yake akaondoka naye.
Ndipo yule jogoo Mweupe aliyeshindwa na kujificha
alitoka konani na kutawala zizi akiwa huru asiye na mpinzani.
Hadithi hii
inatufundisha nini?
1……………………………………………………………………………………………………………………
2……………………………………………………………………………………………………………………
3……………………………………………………………………………………………………………………
Taja methali, nahau au
msemo wa Kiswahili wenye maana inayofanana na maudhui ya hadithi
hii;
………………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………………
0 maoni:
Chapisha Maoni