Hadithi za kale zenye mafundisho za Esopo zilizoandikwa zaidi ya miaka 3000 iliyopita. Zimetafsiriwa kwa Kiswahili na Issa S. Kanguni, chini ya shirika lisilo la kiserikali la Tanzania Inventors and Techno-Thinkers Consortium (TITC). Tel; +255757242960

Tafuta katika Blogu Hii

Pages

Jumamosi, 28 Februari 2015

KISA CHA TAUSI NA KORONGO

Tausi, kwa maringo na madaha aliupepeza mkia wake mpana na kumdhihaki Korongo ambaye alikuwa akipita karibu yake, akimtazama kwa dharau kwa kuona rangi ya manyoya yake iliyofubaa na isiyovutia, akamwambia, 
“Ona mimi nimevikwa joho la kupendeza, kama mfalme vile, kwa rangi ya dhahabu na hudhurungi na rangi nyingine zote za upinde wa mvua; ilhali wewe huna hata punje ya rangi ya kuvutia kwenye mbawa zako.”
Tausi akimtambia Korongo

“Ni kweli,” alijibu Korongo; “lakini mwenzio ninaruka na kupaa kwa raha juu angani huku nikipaza sauti yangu kuelekea anga za mbali kwenye nyota, wakati wewe unanatembea chini tu, kama jogoo, miongoni mwa ndege wala vinyesi.”


FUNDISHO; MANYOYA MAZURI HAYAFANYI NDEGE MZURI.
Share:

Live Traffic Feed

Blogroll

BTemplates.com

Inaendeshwa na Blogger.

Jumla ya Mara Iliyotazamwa

Popular Posts

Kumbukumbu la Blogu