Mtoto mmoja,
akiwa anarudi peke yake kutoka machungani wakati wa jioni, alipita
katikati ya kichaka ambako alikutana na Mbwa mwitu. Kumbe yule Mbwa
mwitu alikuwa na njaa na alijua kuwa mtoto kama yule angetosha kabisa
kwa chakula cha jioni kwake na kwa familia yake ya watoto wanne kule
pangoni. Alianza kumnyemelea akimmezea mate kwa uchu.
Yule...
Jumanne, 31 Desemba 2013
Jumatatu, 30 Desemba 2013
KISA CHA SIMBA NA PANYA
Siku moja
mfalme Simba akiwa amejipumzisha kivulini, alipitiwa na usingizi.
Panya mtukutu alimsogelea na kuanza kuchezacheza juu yake; hali
ambayo ilimfanya aamke mara moja. Alipoamka, Simba alimkamata Panya kwa
kumkandamiza na guu lake kubwa, tayari kwa kumla.
“Naomba
unisamehe, ee Mfalme,” Panya alilia na kuomba: “nisamehe kwa sasa
na sitosahau...
HADITHI YA SEREMALA NA SANAMU YA MEKYURI
Kulikuwa na
mtu mmoja fukara sana, kazi yake ni fundi Seremala. Ndani ya nyumba
yake pamoja na vitu vingine, aliweka sanamu ya Mekyuri ambaye
aliaminika kuwa ni mjumbe wa Mungu.
Kila siku fukara huyo aliitolea
sanamu ile sadaka, na kuiomba imbariki na kumfanya kuwa tajiri.
Lakini fundi alizidi tu kuwa fukara siku hadi siku, zaidi na zaidi.
Mwishowe
alighadhibika,...
HADITHI YA MBWEHA NA PAKA
Mbweha
alikuwa akijigamba mbele ya Paka kuwa yeye ana mbinu nyingi sana za
kuwakwepa maadui zake.
“Nina fuko
zima la mbinu na ujanja,” alisema, “ambalo lina mamia ya njia za
kujiepusha na maadui zangu wakati wa hatari.”
“Mimi
ninayo mbinu moja tu,” alisema Paka; “lakini ninaiamini, na
inanifaa hiyo hiyo.”
Wakiongea
maneno hayo, punde wakasikia...
KISA CHA SUNGURA NA SIMBA
Hapo zamani
za kale kulikuwako mkutano mkuu wa wanyama kila baada ya miaka
mitatu, ambapo wanyama wote walipata fursa ya kutoa michango ya
mawazo ili kuboresha kanuni na namna ya maisha yao kama jamii moja.
Siku moja,
wakiwa katika mkutano kama huo, Sungura walitoa mawaidha kwa hisia
kali sana, rai yao ikiwa ni kutaka wanyama wote wawe na haki...
HADITHI YA SIMBA NA SUNGURA
Simba mwenye
njaa, katika pitapita zake za kuwinda, alimkuta Sungura akiwa amelala
fofofo. Alishusha pumzi, akatabasamu na kumshukuru sana Mungu kwa
ukarimu wake wa kutambua taabiko lake na kumtunuku chakula pasi na
haja ya kukitolea jasho.
Taratibu
alimsogelea Sungura ili asije akamwamsha, akalala yeye…
Alipoinua
miguu yake kutaka kumkamata,...
HADITHI YA MTU NA MTI
Mtu mmoja
alikwenda kichakani huku akiwa na shoka mikononi kwake, na kuiomba
Miti kwa unyenyekevu ili iweze kumpa tawi moja tu dogo ambalo
alisema alikuwa na kazi nalo fulani.
Miti ile
ilikuwa na tabia njema, ikampa moja ya matawi yake. Kumbe yule mtu
alikuwa akihitaji mpini wa shoka lake. Kwa kutumia tawi lile
alilopewa akakarabati shoka lake...
HADITHI YA NYANI NA WANAWE MAPACHA
Ilisemekana
wakati fulani kuwa Nyani mmoja alikuwa akizaa watoto wawili mapacha
katika kila mzao wake. Na alikuwa na kasumba ya kumpenda na kumjali
sana mtoto mmoja, yule mdogo, huku akimchukia na kutomjali kabisa yule
mkubwa.
Ikatokea katika mzao wake mmoja kwamba yule mdogo
aliyempenda na kumjali akasongwasongwa na kudhoofika kiafya na
kimaadili...
KISA CHA SIMBA, MBWA MWITU NA MBWEHA
Simba,
kutokana na uzee wake, alilala akiwa hoi mgonjwa kwenye pango lake.
Wanyama wote wa mwituni walikwenda kumwona na kumsalimu mfalme
wao, isipokuwa Mbweha. Kwahiyo Mbwa mwitu, ambaye walikuwa na uhasama
wa jadi na Mbweha, aliwaza kuwa huo ulikuwa ni wasaa mzuri sana wa
kumkomoa. Akabuni hila ya kutoa mashtaka kwa Mfalme Simba kwamba...
KISA CHA MWANAFALSAFA, MCHWA NA MEKYURI
Hapo zamani
za kale, Mwanafalsafa mmoja alikuwa na kawaida ya kwenda ufukweni mwa
bahari kila siku nyakati za jioni, kujipumzisha na kutafakari.
Ikatokea alasiri ya jumamosi moja, akiwa ufukweni kama ilivyo ada
yake, alishuhudia kwa macho yake mashua ikipigwa na dhoruba kali
na kuzama.
Mabaharia na abiria wote waliokuwamo chomboni walizama...
Jumatatu, 23 Desemba 2013
KISA CHA MBWEHA, JOGOO NA MBWA
Kulitokea
usiku mmoja wa mbalamwezi Mbweha alikuwa akizungukazunguka kwa
mawindo kwenye shamba la Mkulima mwenye mifugo, ambapo aliliona
Jimbi moja limesimama juu kabisa asipoweza kufikia likiwika kwa sauti
ya juu.
“Habari
njema, habari njema!” Mbweha alipaza sauti kwa hila.
“Nijuze, ni
ipi habari hiyo njema?” Jimbi lilijibu.
“Mfalme
Simba...
KISA CHA MWANAMFALME NA PICHA YA SIMBA
Hapo zamani
kulikuwako Mfalme, ambaye alikuwa na mtoto mmoja tu wa kiume, kijana
aliyependa sana mazoezi ya sanaa za mapigano. Kila siku
alijichanganya na vijana wa rika lake katika mazoezi na michezo. Na
awapo nyumbani alipendwa sana na wazazi wake, hasa baba yake.
Siku moja
Mfalme akiwa usingizini aliota ndoto. Na katika ndoto hiyo alipewa
onyo...
KISA CHA KIJANA NA UPUPU
Hapo zamani
kulikuwa na Kijana mmoja mtukutu ambaye alipenda sana kuchezea mimea
na wadudu. Siku moja akiwa kwenye kichaka jirani na nyumbani kwake,
aligusa Upupu kwa mkono wake wa kuume, nao ukaanza kumwasha.
Ukamletea karaha na maumivu makali.
Akaamua
kukimbilia nyumbani kwake haraka huku akiendelea kujikuna na machozi
yakimlengalenga. Alimfuata...
KISA CHA SUNGURA NA MBWEHA
Hapo zamani
za kale Sungura walianzisha vita na Tai. Mapambano yalianza na kila
upande ukijigamba na kudhani ulikuwa na uwezo wa kumshinda mwenzie.
Vita
vilipopamba moto, Sungura walihisi kuzidiwa. Baada ya vikao na
mashauriano ya majemedari, walikubaliana kutuma maombi kwa Mbweha
ili waje kama mamluki kuwasaidia kupambana na jeshi shupavu la...
KISA CHA MAJOGOO WAWILI NA MWEWE
Majogoo
wawili walioishi kwenye zizi moja walianza kupigana wakigombea ukuu
katika himaya yao. Mwishowe jogoo Mwekundu alimshinda jogoo Mweupe,
ambaye alisalimu amri na kukimbia.
Jogoo Mweupe
alienda kujificha kwenye kona ya mbali kwa unyonge, ilhali yule
Mwekundu aliyeshinda alirukia juu ya ukuta, akapiga mbawa zake na
kuwika kwa sauti kuu kama...
KISA CHA CHURA MTABIBU
Hapo zamani
za kale kulikuwako Chura mkubwa.
Siku moja
Chura huyo alijitokeza toka nyumbani kwake Kidimbwini Maguguni na
kuwatangazia wanyama wote kwa kujitapa kwamba yeye ni mtabibu mjuzi,
na ni mbobevu katika masuala ya tiba na dawa. Akatembea kifua mbele
na kujigamba kuwa ana uwezo wa kutibu magonjwa ya aina zote, kwa
jamii zote za wanyama!
Mbweha...
KISA CHA POPO, NDEGE NA WANYAMA
Hapo zamani
za kale kulitokea mgogoro mkubwa sana kati ya Ndege na Wanyama, na
vita kati yao ilinukia. Ilionekana kana kwamba juhudi zote za
mapatano ziligonga mwamba. Wakati majeshi hayo mawili yakijikusanya
kujiandaa kwa mapigano ya umwagaji damu, Popo alisita kuchagua upande
wa kujiunga nao kivita.
Jeshi la
Ndege lilipita karibu na kitulio chake...
KISA CHA KIJANA MWINDA SENENE
Kijana mmoja
mdogo alikuwa akidaka Senene kwenye majani yaliyomea kando ya shamba
lao. Ilikuwa ni mapema wakati wa asubuhi, hata umande ungali
haujavukizwa. Baada ya nusu saa tu alifanikiwa kuwadaka Senene wengi
sana. Wakati akijiandaa kurudi nyumbani, alitupa macho huku na huko
na kumwona Nge akiwa amejipachika katikati ya majani mawili. Basi
yule...
KISA CHA SUNGURA NA VYURA
Sungura
walikuwa wakionewa sana na wanyama wengine kwa kupigwa, kuwindwa na
kuliwa, kiasi kwamba hawakujua wakimbilie wapi. Ikawa wanaishi maisha
ya karaha mno na kila walipomwona mnyama yeyote akiwakaribia,
walilazimika kutimua mbio kwa woga.
Siku moja
wakaliona kundi la Farasi pori walio katika hali ya taharuki
wakikimbia na kuwaelekea wao. Walihamaki...
KISA CHA SIMBA NA PAPA
Siku moja
Simba alikuwa akirandaranda ufukweni mwa bahari, akamwona Papa
akichomoza kichwa chake juu ya uso wa bahari katikati ya mawimbi.
Alizama na kuibuka tena… akazama na kuibuka tena… Simba alivutiwa
naye na kumwona kuwa anafaa kuwa rafiki kwani ni mkubwa na mwenye
nguvu kama yeye.
Alimwita
karibu naye akasogea.
Baada ya
kusalimiana Simba...
KISA CHA MBWEHA NA MBU
Siku moja,
baada ya kutembea kwa muda mrefu, Mbweha aliukuta mto mdogo wenye
kina kifupi cha maji. Maji yalikuwa masafi na maangavu kabisa na
mandhari ya bonde lile kwa ujumla ilikuwa ya kuvutia kutokana na uoto
na magugu yaliyonawiri vizuri pembezoni. Akayatamani maji kwa uzuri
wake japo hakuwa na kiu kabla, akayanywa, kisha akatulia kidogo kwa
tafakuri.
Hapohapo
akapata...
KISA CHA SUNGURA NA MBWA
Katika
pitapita zake za mawindo, Mbwa alimvumbua Sungura kwenye maficho
yake. Akaanza kumkimbiza. Baada ya kukimbizana kwa muda mrefu, Mbwa
alishindwa kumkamata kutokana na Sungura kumpiga chenga lukuki za
maudhi. Akaamua kusimama.
Kundi la
Mbuzi lilikuwapo mahali pale na walishuhudia kinagaubaga sakata hilo.
Ikawa burudani kwao kwani mioyoni...
KISA CHA MBUZI NA MCHUNGAJI
Mchunga
Mbuzi alihangaika kumrudisha Mbuzi mmoja aliyetoka kundini na kuingia
kwenye shamba la jirani. Alipiga mbinja na kupuliza baragumu bila ya
mafanikio; yule Mbuzi alimbeza na kuidharau miito yote.
Mwishowe Mchunga Mbuzi aliudhika na kumrushia jiwe kwa nguvu,
likamvunja pembe moja.
Kuona vile Mchunga Mbuzi alipagawa kwa...
KISA CHA BABU KIZEE NA KIFO
Babu kizee
mmoja aliajiriwa kufanya kazi ya kukata magogo ya miti msituni. Siku
moja akiwa anarejea nyumbani jioni alibebeshwa mzigo wa kuni aupeleke
mjini ukauzwe. Mzigo ule ulikuwa mzito sana kwake.
Baada ya
mwendo wa kitambo kirefu alichoka akawa hoi kabisa. Alisononeka kwa
ufukara wake unaopelekea apate mateso ya kufanya kazi mzito mchana
kutwa,...
KISA CHA AYALA NA MZABIBU
Ayala, baada
ya kukimbizwa na kuandamwa na wawindaji toka mbali, alichoka sana na
kujua sasa mwisho wake umefika. Wawindaji walipomkaribia alifanya
hila, akachupa kuume na kujibanza kwenye mvungu wa majani makubwa ya
Mzabibu.
Wawindani nao kwa haraka waliyokuwa nayo (na hulka ya kuwahi ni
kupata) hawakuweza kuing’amua hila yake, wakampita palepale...
KISA CHA MAKSAI NA WACHINJA NG'OMBE
Maksai, hapo
zamani za kale, waliazimia kufanya hila ya kuwashambulia ghafla na
kuwaangamiza Wachinja ng’ombe wote, kwa kuwa walikuwa wanaendesha
biashara inayoteketeza jamii yao. Azimio hilo lilipitishwa kwa wingi
mkubwa wa kura na maandalizi ya utekelezaji wake yakaanza mara moja.
Siku ya siku
ilipofika walikusanyika ili waweze kutekeleza azma...
Jumamosi, 21 Desemba 2013
KISA CHA MJAKAZI NA NYOKA
Hapo zamani
za kale, kulikuwapo Nyoka mkubwa mwenye sumu kali, ambaye aliweka
makazi yake kwenye shimo pembezoni mwa baraza ya nyumba ya Mjakazi
mmoja. Siku moja usiku wa manane yule Nyoka alimng’ata mtoto
mchanga wa Mjakazi, mwili wake ukabadilika rangi kuwa mweusi tii,
akafa.
Kukawa msiba
na simanzi isiyo kifani.
Wakati
akiomboleza kifo cha...
KISA CHA NGURUWE, KONDOO NA MBUZI
Nguruwe mmoja
mdogo alikuwa amefungiwa kwenye uzio wa miti. Mbuzi na Kondoo pia
walifungwa pamoja naye. Siku moja Mchungaji wao alikuja na kumkamata
yule Nguruwe, ambaye aliguna na kuanza kupiga kelele na kufurukuta.
Mbuzi na
Kondoo walimlalamikia Nguruwe kwa kelele zake za kilio na
purukushani, wakasema kwa kejeli, “Mara kwa mara Mchungaji...
KISA CHA MVUVI NA SAMAKI MDOGO
Ilitokea siku
moja kuwa, Mvuvi, baada ya kuhangaika kwenye kazi yake ya kuvua kutwa
nzima, aliambulia kukamata Samaki mmoja tu mdogo.
Yule Samaki
akamwambia Mvuvi kwa kumbembeleza;
“Tafadhali
niachie ee bwana,” alilalamika. “Mimi bado ni mdogo sana,
sijafikia rika ya kuliwa nawe kwa sasa. Ukinihurumia na kunirudisha
mtoni, nitakua haraka, na ndipo...
KISA CHA MWANAKONDOO NA MBWA MWITU
Mbwa mwitu
alimkimbiza Mwanakondoo, ambaye ili kujiokoa alikimbilia ndani ya
hekalu moja la ibada. Mbwa mwitu hakuweza kuingia hekaluni, badala
yake alisimama nje akapaza sauti kumwita akimwambia, “Ni heri uje
kwangu, maana humo ulimokimbilia Padre akikukamata atakuchinja na
kukufanya dhabihu.”
Mwanakondoo akamjibu, “Ni heri nitolewe kafara ndani
ya...