Hadithi za kale zenye mafundisho za Esopo zilizoandikwa zaidi ya miaka 3000 iliyopita. Zimetafsiriwa kwa Kiswahili na Issa S. Kanguni, chini ya shirika lisilo la kiserikali la Tanzania Inventors and Techno-Thinkers Consortium (TITC). Tel; +255757242960

Tafuta katika Blogu Hii

Pages

Jumatatu, 16 Juni 2014

KISA CHA NYANI WACHEZA SHOO

Mwanamfalme aliagiza Nyani kadhaa wapewe mafunzo maalum ya kucheza shoo. Kwa  vile kwa asili Nyani ni waigaji wazuri sana wa matendo ya binadamu, walionyesha kuwa wanafunzi bora wenye kushika mafuzo haraka, na walipovishwa nguo na vinyago kichwani, walicheza...
Share:

Kisa cha Wavulana na Vyura

Watoto wavulana, wakiwa wanacheza kandokando ya bwawa, waliona Vyura kwenye maji wakaanza kuwarushia mawe huku wakifurahia mchezo wa kulenga shabaha.  Waliwaua vyura kadhaa, hadi Chura mmoja jasiri, alipotokeza kichwa chake nje ya maji, na kuwaambia kwa uchungu:  "Acheni,...
Share:

Kisa cha Mbwa na Mbweha

Mbwa, katika pitapita zao waliikuta ngozi ya Simba, wakaanza kuing'ata na kuirarua vipande vipande kwa meno yao.  Mbweha aliwaona, akawaambia,  "Laiti kama Simba huyo angekuwa hai, basi bila shaka mngetambua ya kuwa makucha yake yana nguvu kuliko...
Share:

Jumamosi, 31 Mei 2014

KISA CHA NYIGU NA NYOKA

Nyigu alitua kwenye kichwa cha Nyoka na kuanza kumng’ata mfululizo, akimjeruhi vibaya kwa lengo la kutaka kumwua.  Nyoka, akiwa katika maumivu makali asijue namna ya kujiokoa na adui yake huyo, mara akaona mkokoteni uliojazwa magogo ya miti ukipita.  Basi kwa...
Share:

KISA CHA MITUNGI MIWILI

Mitungi miwili iliachwa kwenye ukingo wa mto, mmoja wa chuma, na mwingine wa udongo.  Baada ya mvua kubwa kunyesha mbali mto utokako ndipo maji ya mto yalipoongezeka na hatimaye mitungi yote ilisombwa ikaelea kufuata mkondo.  Basi ule mtungi wa udongo ukawa unafanya...
Share:

Ijumaa, 30 Mei 2014

KISA CHA MAADUI WAWILI

Jamaa wawili, ambao walikuwa ni maadui wa kufa na kupona, walijikuta wakisafiri katika merikebu moja. Wakiwa wamepania kukaa mbalimbali kadri iwezekanavyo, mmoja alienda kukaa nyuma kabisa na  mwingine mbele kabisa kwenye ncha ya mwisho ya merikebu.  Mara kukapiga dhoruba kali na mawimbi yakaanza kukipeleka chombo mrama, na kilipokuwa...
Share:

KISA CHA PANYA WA MJINI NA PANYA PORI

Panya Pori alimwalika panya wa mjini, ambaye ni rafiki yake kipenzi, amtembelee kwake aje ajionee maisha ya porini. Wakiwa kwenye uwanda wazi wa mashamba, wakila mabaki ya nafaka na mizizi ya miti iliyong’oka, Panya wa Mjini alimwambia rafiki yake,   “Huku shamba...
Share:

KISA CHA MBWA WAWILI

Kulitokea bwana mmoja ambaye alifuga mbwa wawili:  Mbwa mwindaji, ambaye alimfundisha kumsaidia katika kazi zake za uwindaji, na Mbwa mlinzi, aliyemfundisha kulinda nyumba.  Kila aliporejea nyumbani kutoka mawindoni, alikuwa akimpa yule Mbwa wa nyumbani minofu...
Share:

Alhamisi, 22 Mei 2014

Kisa cha Bwana Mzalendo mwenye Kipawa

Baada ya kufanikiwa kupewa nafasi ya kusikilizwa na mfalme na baraza lake la washauri, Mzalendo mwenye kipaji alitoa karatasi mfukoni mwake, akasema:  ::soma zaid...
Share:

Jumapili, 18 Mei 2014

KISA CHA TAI, PAKA NA NGURUWE PORI

Kulitokea Tai mmoja ambaye alijenga kiota chake juu ya mti mkubwa; Paka naye, baada ya kuona kuna shimo linalomfaa, alihamia na kuanza kuishi katikati ya shina la mti ule ule; na Nguruwe pia, akiwa na vitoto vyake, akaweka makazi kwenye shimo lililopo wazi chini ya mti ule.  Basi...
Share:

KISA CHA MARAFIKI WAWILI NA DUBU

Marafiki wawili walikuwa wakisafiri pamoja kupitia vichakani, mara akatokea dubu mkubwa na kuanza kuwakimbiza. Katika harakati za kutaka kujiokoa walikimbia na ikawa mmoja kati yao alikuwa mbele na mwingine nyuma yake.  Basi yule wa mbele iliwahi kulishika tawi la...
Share:

Jumamosi, 17 Mei 2014

KISA CHA BAHILI NA DHAHABU ZAKE

Bwana mmoja bahili aliuza vitu vyake vyote alivyonavyo na kununua sarafu za dhahabu, ambazo alichimba shimo na kuzifukia chini kando ya ukuta wa zamani na kuwa anakwenda kuziangalia kila siku. Mmoja wa wafanyakazi wake aligundua safari zake za mara kwa mara kwenda eneo lile...
Share:

KISA CHA MBWA NA MBWA MWITU

Mbwa-mwitu mmoja dhaifu alikuwa akikaribia kufa kwa njaa na mara kwa bahati akakutana na mbwa wa nyumbani ambaye alikuwa akipita.  "Ah, binamu," alisema mbwa "nilijua tu yatakukuta haya; kwamba maisha yako ya kutangatanga na yasiyo na uhakika ipo siku yatakuangamiza....
Share:

KISA CHA MBWA NA SUNGURA

Mbwa mwindaji alimvumbua Sungura kwenye mafukutu juu ya kilima na kuanza kumkimbiza kwa kitambo, wakati fulani alimkaribia na kung'ata kwa nguvu kwa meno yake makali kana kwamba ataka kumuua, na mara nyingine alimkumbatia kana kwamba anacheza na mbwa mwenzake.  Yule...
Share:

KISA CHA MZEE KIPARA NA MBUNG'O

Mbung'o alitua kichwani kwa Mzee mmoja na kumng'ata kwenye sehemu yenye kipara, ambapo yule Mzee kwa kutaka kumwangamiza Mbung'o alijipiga kofi pwaaa!  Yule mbung'o alifanikiwa kukwepa na aliondoka akisema kwa dhihaka,  "Ulipanga kulipiza kisasa, hata kwa kuua,...
Share:

KISA CHA MAMA NA MTETEA

Hapo zamani za kale kulikuwako mama mmoja ambaye alikuwa na kuku wake mtetea aliyetaga yai moja kila siku.  Kila wakati yule mama alifikiri na kujiuliza atawezaje kupata mayai mawili kwa siku badala ya moja, na mwishowe, ili kutimiza azma yake, akaamua kuanza kumlisha...
Share:

KISA CHA MBWEHA ALIYEKATWA MKIA

Hapo zamaini za kale, kulitokea Mbweha mmoja mjanja. Siku moja kwenye pitapita zake kwa bahati mbaya alinaswa mtegoni, na katika kuhangaika alifanikiwa kujinasua, ila alikatika mkia ukabakia kipisi kifupi tu. Siku za mwanzo mwanzo aliona aibu kujionyesha ulemavu wake wa kutokuwa na mkia kwa mbweha wenzake. Baadaye akaamua kujibaraguza na kufanya...
Share:

Jumatano, 7 Mei 2014

KISA CHA MBWEHA, MBWA MWITU NA NYANI

Mbwa mwitu alimshutumu  vikali Mbweha kwa kumwibia, ila Mbweha alikana katukatu kwamba hakutenda kosa hilo. Baada ya kuzozana kwa muda, wakampelekea Nyani shauri hilo ili atoe hukumu na kumaliza mgogoro baina yao.  Basi baada ya kila mmoja wao kupewa nafasi ya kujieleza kwa kina, Nyani akatangaza hukumu ifuatayo:  "Siamini katu...
Share:

KISA CHA WASAFIRI WAWILI NA SHOKA

Jamaa wawili walikuwa wakisafiri pamoja. Wakiwa njiani mmoja wao aliokota shoka zuri lililokuwa limelazwa kando ya njia, akalichukua na kusema,  "Nimeokota shoka."  "Hapana rafiki yangu," mwenzake alimjibu, "usiseme 'Nimeokota' bali 'Tumeokota' shoka."  Basi...
Share:

Jumatano, 30 Aprili 2014

MIFUKO YA DHAMBI

Kwa mujibu wa masimulio ya ngano za kale za mababu zetu, eti inasemekana kwamba kila binadamu hapa duniani amezaliwa na mifuko miwili ikining'inia shingoni mwake.  Fuko kubwa la mbele linajazwa mapungufu na madhambi ya majirani zake, na fuko kubwa linaloning'inia nyuma linajazwa mapungufu na madhambi yake mwenyewe.  Ndiyo maana watu...
Share:

KISA CHA MWINDAJI NA MVUVI

Mwindaji, akiwa na mbwa wake anarejea kutoka mawindoni, kwa bahati alikutana na Mvuvi ambaye naye alikuwa anarejea nyumbani toka ziwani na kapu lake lililojaa samaki.  Basi ikawa yule Mwindaji akatamani sana wale samaki kwenye kapu la Mvuvi, ilhali yule Mvuvi naye...
Share:

KISA CHA MPIGA-TARUMBETA VITANI

Hapo zamani za kale, kulikuwapo bwana mmoja mpiga tarumbeta ambaye alikuwa jasiri akiwaongoza askari  vitani.  Basi siku moja huku vita ikiwa imepamba moto, alisogea kuwakaribia maadui kupita kiasi, matokeo yake akakamatwa. Wakati wakijiandaa kumnyonga, akaanza kulia na kubembeleza asiuawe na badala yake aachiwe huru, "Tafadhalini niacheni,...
Share:

Jumapili, 27 Aprili 2014

KISA CHA WEZI NA JOGOO

Vibaka walivunja nyumba ili wakaibe na walipoingia ndani hawakukuta kitu chochote isipokuwa jogoo. Wakamkamata jogoo yule na kuondoka naye haraka.  Walipofika kwao walijiandaa kumchinja jogoo watengeneze kitoweo, ambapo jogoo alianza kujitetea asiuawe: “Tafadhalini msinichinje; ni vyema mkanifuga kwani ninasaidia sana watu. Ninawaamsha watu...
Share:

KISA CHA KIBAKA NA MAMAYE

Hapo zamani za kale kulikuwepo mvulana mmoja aliyeishi na mama yake. Siku moja, akiwa shuleni kijana aliiba kitabu cha mwanafunzi mwenzake na kurudi nacho nyumbani akamwonyesha mama yake. Yule mama, sio tu hakumchapa wala kumgombeza, bali alimpongeza.  Kijana akakua kuelekea utu uzima, huku akiendelea na tabia yake ya wizi wa vitu vikubwa...
Share:

Jumatano, 23 Aprili 2014

NIPE RISITI - La Sivyo...

Onyo; Hadithi hii ni ya kubuni (fiction) na haina uhusiano na tukio lolote lililowahi kutokea. Majina ya wahusika na tabia zao hazina uhusiano na mtu yeyote halisi hivyo ikitokea aina yoyote ya kufanana ni bahati mbaya tu.  Mtunzi; Issa S. Kanguni 0757242960...
Share:

Jumapili, 20 Aprili 2014

KISA CHA NJIWA MWENYE KIU

Njiwa, akiwa amezidiwa na kiu kupita kiasi, aliona picha ya mtungi wa maji iliyochorwa kwenye bango.  Basi bila kuangalia kwa makini, aliruka kwa pupa kuulekea mtungi huku akipiga kelele ya shangwe, pasi kujua kuwa ule ni mchoro tu.  Matokeo yake akajibamiza...
Share:

KISA CHA BWANA MWENYE WAKE WAWILI

  Hapo zamani za kale, kulitokea bwana mmoja wa makamo ambaye alikuwa na wake wawili, mmoja mtu mzima na mwingine kijana; ambapo wote walimpenda sana, na kila mmoja alitamani awe anaendana naye.  Na kwa wakati ule yule bwana nywele zake zilianza kuota mvi, jambo ambalo mke mdogo hakupendezwa  nalo, kwani lilimfanya aonekane ameolewa...
Share:

Kisa cha Simba Aliyezama Kwenye Mapenzi

Hapo zamani za kale, Simba, mfalme wa mwitu, alitokea kumpenda binti mzuri wa jamaa mmoja mkata miti. Akapeleka maombi ya kinguvu ya kutaka amwoe. Baba wa binti yule, hakupenda kuruhusu mwanaye aposwe na mfalme Simba, lakini pia aliogopa kukataa ombi hilo.  Akajikuta...
Share:

Alhamisi, 30 Januari 2014

HADITHI YA BIBI KIZEE NA CHUPA YA MVINYO

Bibi kizee aliokota chupa tupu ya mvinyo ambayo alitambua kuwa siku nyingi zilizopita ilijaa mvinyo. Ila alishangaa kuona kuwa hadi wakati huo ilikuwa ikitoa harufu mzuri ya kinywaji hicho. Kwa uchu, aliisogeza chupa hiyo puani na kuvuta harufu yake, akaitazama, kisha akarudia kuinusa mara kadhaa na kusema kwa husuda, “Oo… kinywaji murua kabisa!...
Share:

KISA CHA NG'OMBE NA CHURA

Ng’ombe Maksai alikwenda kunywa maji katika dimbwi ambalo lilikuwa na watoto wa chura. Watoto hao walizaliwa hapo na kwao hiyo ilikuwa ni maskani yao halali. Ila kwa wakati ule mama yao alikuwa ametoka, kaenda kuitembelea familia ya rafiki yake iliyokuwa na makazi kwenye dimbwi jingine upande wa pili wa kichaka. Kwa bahati mbaya, Maksai alimkanyaga...
Share:

Alhamisi, 2 Januari 2014

HADITHI YA MBWEHA NA CHUI

Siku moja mbweha na chui walizozana kuhusu nani kati yao alikuwa mzuri kuliko mwenzake. Chui alijinadi kwa kumwonyesha mbweha moja baada ya jingine madoa yaliyoipamba na kuipendezesha ngozi yake. Na kweli ukimwangalia Chui na madoa yake alionekana mzuri anayevutia. Lakini mbweha naye alimkatiza kwa kusema, “hivi ni nani mzuri kati yako wewe,...
Share:

KISA CHA MWANADAMU NA SIMBA

Mwanadamu na Simba walikuwa wakisafiri pamoja kuelekea upande mwingine wa nchi. Wakiwa safarini walianza kutambiana, kila mmoja akijigamba kuwa ni mkuu na mwenye ushujaa na umahiri. Wakati wakiendelea kubishana, walipita mahali ambapo kulikuwa na sanamu kubwa ya mawe ikimwonyesha...
Share:

KISA CHA MCHEKESHAJI NA MWANAKIJIJI

Hapo zamani kulikuwepo mtu mmoja tajiri aliyeheshimika sana na watu wa jamii yake. Bwana huyo alifungua majumba ya maonyesho ya sanaa na watu wote waliruhusiwa kuingia bure. Wake kwa waume, watoto na wakubwa. Ikawa baada ya kazi nyingi za kutwa za kujitafutia riziki, Wananchi wakapata burudani na kufurahi pamoja. Ila kwa kuwa maonyesho yalifanyika...
Share:

HADITHI YA TAI NA MBWEHA

Tai na Mbweha walikuwa marafiki wapenzi na hivyo walikubaliana kutoishi mbalimbali. Wakautafuta mti mmoja mzuri. Tai akajenga kiota chake kwenye matawi ya mti huo mkubwa, wakati Mbweha aliweka makazi yake kwenye shimo chini ya mti huo huo. Miezi michache baadaye Mbweha alizaa vitoto vinne. Muda si mrefu baada ya makubaliano yao ya kuishi jirani...
Share:

KISA CHA MUUAJI

Mtu mmoja alimjeruhi mwenzie na kumuua. Ndugu na jamaa wa marehemu walianza kumkimbiza wakiwa na silaha kwa minajili la kumuua kwa kisasi. Yule muuaji alikimbia kwa bidii kuu ili aokoe roho yake na hatimaye akafika kwenye kingo ya mto Nile. Ng’ambo ya mto alimwona Simba na kwa woga wake wa kuhofia kuuawa akaamua kukwea juu ya mti.  Kule...
Share:

HADITHI YA SIMBA, MBWEHA NA WANYAMA WENGINE

Siku moja Simba alitangaza kuwa yu mgonjwa mahtuti na kwamba alikaribia kufa. Hivyo alitoa tamko la kuwaalika Wanyama wote waende nyumbani kwake kumwona na kusikia wosia wake wa mwisho na ushuhuda wa mambo kadha wa kadha, na pia wapate busara za mfalme. Hivyo Mbuzi alienda kwenye pango alililoishi Mfalme Simba ili kumjulia hali. Alisimama kwenye...
Share:

Live Traffic Feed

Blogroll

BTemplates.com

Inaendeshwa na Blogger.

Jumla ya Mara Iliyotazamwa

183410

Popular Posts