Tai
na Mbweha walikuwa marafiki wapenzi na hivyo walikubaliana kutoishi
mbalimbali. Wakautafuta mti mmoja mzuri. Tai akajenga kiota chake
kwenye matawi ya mti huo mkubwa, wakati Mbweha aliweka makazi yake
kwenye shimo chini ya mti huo huo. Miezi michache baadaye Mbweha
alizaa vitoto vinne.
Muda
si mrefu baada ya makubaliano yao ya kuishi jirani kwa urafiki, Tai,
kutokana na mahitaji yake ya chakula cha kuwalisha makinda wake,
alishuka chini ya mti wakati rafiki yake Mbweha yupo matembezini,
akakamata kitoto kimoja cha Mbweha, akakiua na kukila yeye na wanawe.
Mbweha
aliporudi, aligundua kilichotokea, akahuzunika sana. Huzuni yake kuu
haikuwa tu kwa kifo cha mtoto wake, bali pia ni jinsi ambavyo hakuwa
na uwezo wa kulipiza kisasi kwa ukatili aliofanyiwa na rafiki yake,
kwani asingeweza kupanda juu kwenye kiota cha Tai.
Hata hivyo
muda si mrefu baadaye malipo ya udhalimu yalimfika Tai.
Akirukaruka
kwenye mawindo sehemu fulani , ambako wanakijiji walikuwa wakitoa
dhabihu ya mbuzi, ghafla akashuka na kudokoa pande la nyama, na
kulichukua, pamoja na kizinga cha moto kilichoambatana nayo, bila
kujua hadi kwenye kiota chake. Upepo mkali uliopovuma uliwasha moto
kwenye kiota, hivyo wale makinda wake, kwa kuwa hawakuwa na mbawa
bado, walishindwa kujiokoa wakaungua na kubanikwa kwenye kiota chao
wakafa na kudondoka chini ya mti.
Hapo chini, huku mama yao Tai
akishuhudia, Mbweha akawala wote kwa kisasi.
Naye Tai alihuzunika sana.
Hadithi hii
inatufundisha nini?
1……………………………………………………………………………………………………………………
2……………………………………………………………………………………………………………………
3……………………………………………………………………………………………………………………
Taja methali, nahau au
msemo wa Kiswahili wenye maana inayofanana na maudhui ya hadithi
hii;
………………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………………
0 maoni:
Chapisha Maoni