Mbwa mwitu alimshutumu vikali Mbweha kwa kumwibia, ila Mbweha alikana katukatu kwamba hakutenda kosa hilo. Baada ya kuzozana kwa muda, wakampelekea Nyani shauri hilo ili atoe hukumu na kumaliza mgogoro baina yao.
Basi baada ya kila mmoja wao kupewa nafasi ya kujieleza kwa kina, Nyani akatangaza hukumu ifuatayo:
"Siamini katu kwamba wewe, Mbwa mwitu, umepotelewa na hicho unachodai kuibiwa; na ninaamini kabisa kwamba wewe, Mbweha, umeiba hicho unachokataa katakata kuwa hujaiba."
***
Hadithi hii inatufundisha nini? Jibu ujishindie.
0 maoni:
Chapisha Maoni