Mitungi miwili iliachwa kwenye ukingo wa mto, mmoja wa
chuma, na mwingine wa udongo.
Baada ya mvua kubwa kunyesha mbali mto utokako ndipo maji ya mto yalipoongezeka na hatimaye mitungi yote ilisombwa
ikaelea kufuata mkondo.
Basi ule mtungi wa udongo ukawa unafanya jitihada
kwelikweli kujiweka mbali na ule wa chuma. Kuona vile, Mtungi wa chuma ukatabasamu na kuuambia
ule wa udongo:
“Usihofu rafiki yangu, mi sikugongi.”
“Sawa, lakini inawezekana nikagusana nawe,” ukasema mtungi wa
udongo, “iwapo nitakukaribia; kwani haijalishi wewe ukinigonga, au mimi
nikakugonga, nitadhurika tu.”
***
0 maoni:
Chapisha Maoni