Mtu mmoja
alimjeruhi mwenzie na kumuua. Ndugu na jamaa wa marehemu walianza
kumkimbiza wakiwa na silaha kwa minajili la kumuua kwa kisasi.
Yule muuaji
alikimbia kwa bidii kuu ili aokoe roho yake na hatimaye akafika
kwenye kingo ya mto Nile. Ng’ambo ya mto alimwona Simba na kwa woga
wake wa kuhofia kuuawa akaamua kukwea juu ya mti.
Kule mtini pia
aliona Joka kubwa kwenye matawi ya juu kwenye kilele, akaogopa sana
kuuawa kwa sumu. Akaamua kujitupa mtoni ambako nako kulikuwa na
Mamba.
Alishikwa akauawa na kuliwa papo hapo.
Hivyo ardhi, anga na maji vyote kwa pamoja vilikataa
kumficha Mwuaji yule.
Hadithi hii
inatufundisha nini?
1……………………………………………………………………………………………………………………
2……………………………………………………………………………………………………………………
3……………………………………………………………………………………………………………………
Taja methali, nahau au
msemo wa Kiswahili wenye maana inayofanana na maudhui ya hadithi
hii;
………………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………………
0 maoni:
Chapisha Maoni