Mwanadamu na
Simba walikuwa wakisafiri pamoja kuelekea upande mwingine wa nchi.
Wakiwa safarini walianza kutambiana, kila mmoja akijigamba kuwa ni
mkuu na mwenye ushujaa na umahiri.
Wakati
wakiendelea kubishana, walipita mahali ambapo kulikuwa na sanamu
kubwa ya mawe ikimwonyesha “Simba akinyongwa na binadamu.”
Msafiri yule alimwonyesha Simba sanamu ile na kusema kwa majivuno:
“Unaona!... jinsi ambavyo binadamu tuna nguvu, na jinsi tunavyoweza
kumshinda hata mfalme wa wanyama wote.”
Simba akamjibu: “Sikiliza rafiki yangu nikupashe,
Sanamu hii tuionayo mbele yetu imechongwa na mmoja kati ya Binadamu.
Laiti kama nasi Simba tungelikuwa na ujuzi wa kuchonga sanamu,
ungeona sanamu ya Binadamu akiwa amefinywa chini ya kiganja cha
Simba.”
Hadithi hii inatufundisha
nini?
1……………………………………………………………………………………………………………………
2……………………………………………………………………………………………………………………
3……………………………………………………………………………………………………………………
Taja methali, nahau au
msemo wa Kiswahili wenye maana inayofanana na maudhui ya hadithi
hii;
………………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………………
0 maoni:
Chapisha Maoni