Kulitokea bwana mmoja ambaye alifuga mbwa wawili:
Mbwa
mwindaji, ambaye alimfundisha kumsaidia katika kazi zake za uwindaji, na Mbwa
mlinzi, aliyemfundisha kulinda nyumba.
Kila aliporejea nyumbani kutoka
mawindoni, alikuwa akimpa yule Mbwa wa nyumbani minofu mikubwa mikubwa ale.
Mbwa mwindaji hakupendezwa na jambo lile na alishindwa kuvumilia, alimfuata
mwenzie, akamwambia,
“Ni mateso makubwa kufanya kazi ngumu kama nifanyayo mimi,
ilhali wewe, ambaye husaidii lolote katika kuwinda, unajibarizi na kufaidi
matunda ya jasho langu.”
Mbwa wa nyumbani akamjibu,
“Rafiki yangu, usinilaumu
mimi bali umlaumu bwana wetu, ambaye hajanifundisha mimi kufanya kazi bali
kuishi kwa kutegemea matunda ya kazi za wengine.”
***
0 maoni:
Chapisha Maoni