Hapo zamani za kale, kulikuwapo bwana mmoja mpiga tarumbeta ambaye alikuwa jasiri akiwaongoza askari vitani.
Basi siku moja huku vita ikiwa imepamba moto, alisogea kuwakaribia maadui kupita kiasi, matokeo yake akakamatwa. Wakati wakijiandaa kumnyonga, akaanza kulia na kubembeleza asiuawe na badala yake aachiwe huru, "Tafadhalini niacheni, msiniue nihurumieni kwa kuwa mimi sina hatia" akasema "mimi si mpiganaji, sijaua mtu yeyote, na sina hata silaha. Mi napiga tu tarumbeta hili, na kwa kweli sidhani kama hiyo inamuumiza yeyote kati yenu. Sioni sababu ya nyie kunidhuru!"
"Ingwa haupambani mwenyewe" wakamjibu "lakini unapopiga tarumbeta lako unawahimiza na kuwaongoza watu wako kupambana nasi. Na hiyo ni sababu tosha kukuadhibu."
0 maoni:
Chapisha Maoni