Jamaa wawili, ambao walikuwa ni maadui wa kufa na kupona,
walijikuta wakisafiri katika merikebu moja. Wakiwa wamepania kukaa mbalimbali
kadri iwezekanavyo, mmoja alienda kukaa nyuma kabisa na mwingine mbele kabisa kwenye ncha ya mwisho ya
merikebu.
Mara kukapiga dhoruba kali na mawimbi yakaanza kukipeleka chombo
mrama, na kilipokuwa kwenye hatari ya kuzama, yule jamaa aliyekaa nyuma
akamuuliza nahodha ni upande upi wa merikebu ile ungelianza kuzama kabla
ya mwingine.
Alipomjibu kwamba anaamini
ni upande wa mbele utakaozama kwanza, yule jamaa akasema,
“Kifo hiki hakitokuwa
na mateso kwangu, endapo tu nitafanikiwa kumwona yule rafiki yangu pale akitapatapa na kufa
kabla yangu.”
***
0 maoni:
Chapisha Maoni