Hadithi za kale zenye mafundisho za Esopo zilizoandikwa zaidi ya miaka 3000 iliyopita. Zimetafsiriwa kwa Kiswahili na Issa S. Kanguni, chini ya shirika lisilo la kiserikali la Tanzania Inventors and Techno-Thinkers Consortium (TITC). Tel; +255757242960

Tafuta katika Blogu Hii

Pages

Jumatano, 30 Aprili 2014

MIFUKO YA DHAMBI

Kwa mujibu wa masimulio ya ngano za kale za mababu zetu, eti inasemekana kwamba kila binadamu hapa duniani amezaliwa na mifuko miwili ikining'inia shingoni mwake.  Fuko kubwa la mbele linajazwa mapungufu na madhambi ya majirani zake, na fuko kubwa linaloning'inia nyuma linajazwa mapungufu na madhambi yake mwenyewe.  Ndiyo maana watu...
Share:

KISA CHA MWINDAJI NA MVUVI

Mwindaji, akiwa na mbwa wake anarejea kutoka mawindoni, kwa bahati alikutana na Mvuvi ambaye naye alikuwa anarejea nyumbani toka ziwani na kapu lake lililojaa samaki.  Basi ikawa yule Mwindaji akatamani sana wale samaki kwenye kapu la Mvuvi, ilhali yule Mvuvi naye...
Share:

KISA CHA MPIGA-TARUMBETA VITANI

Hapo zamani za kale, kulikuwapo bwana mmoja mpiga tarumbeta ambaye alikuwa jasiri akiwaongoza askari  vitani.  Basi siku moja huku vita ikiwa imepamba moto, alisogea kuwakaribia maadui kupita kiasi, matokeo yake akakamatwa. Wakati wakijiandaa kumnyonga, akaanza kulia na kubembeleza asiuawe na badala yake aachiwe huru, "Tafadhalini niacheni,...
Share:

Jumapili, 27 Aprili 2014

KISA CHA WEZI NA JOGOO

Vibaka walivunja nyumba ili wakaibe na walipoingia ndani hawakukuta kitu chochote isipokuwa jogoo. Wakamkamata jogoo yule na kuondoka naye haraka.  Walipofika kwao walijiandaa kumchinja jogoo watengeneze kitoweo, ambapo jogoo alianza kujitetea asiuawe: “Tafadhalini msinichinje; ni vyema mkanifuga kwani ninasaidia sana watu. Ninawaamsha watu...
Share:

KISA CHA KIBAKA NA MAMAYE

Hapo zamani za kale kulikuwepo mvulana mmoja aliyeishi na mama yake. Siku moja, akiwa shuleni kijana aliiba kitabu cha mwanafunzi mwenzake na kurudi nacho nyumbani akamwonyesha mama yake. Yule mama, sio tu hakumchapa wala kumgombeza, bali alimpongeza.  Kijana akakua kuelekea utu uzima, huku akiendelea na tabia yake ya wizi wa vitu vikubwa...
Share:

Jumatano, 23 Aprili 2014

NIPE RISITI - La Sivyo...

Onyo; Hadithi hii ni ya kubuni (fiction) na haina uhusiano na tukio lolote lililowahi kutokea. Majina ya wahusika na tabia zao hazina uhusiano na mtu yeyote halisi hivyo ikitokea aina yoyote ya kufanana ni bahati mbaya tu.  Mtunzi; Issa S. Kanguni 0757242960...
Share:

Jumapili, 20 Aprili 2014

KISA CHA NJIWA MWENYE KIU

Njiwa, akiwa amezidiwa na kiu kupita kiasi, aliona picha ya mtungi wa maji iliyochorwa kwenye bango.  Basi bila kuangalia kwa makini, aliruka kwa pupa kuulekea mtungi huku akipiga kelele ya shangwe, pasi kujua kuwa ule ni mchoro tu.  Matokeo yake akajibamiza...
Share:

KISA CHA BWANA MWENYE WAKE WAWILI

  Hapo zamani za kale, kulitokea bwana mmoja wa makamo ambaye alikuwa na wake wawili, mmoja mtu mzima na mwingine kijana; ambapo wote walimpenda sana, na kila mmoja alitamani awe anaendana naye.  Na kwa wakati ule yule bwana nywele zake zilianza kuota mvi, jambo ambalo mke mdogo hakupendezwa  nalo, kwani lilimfanya aonekane ameolewa...
Share:

Kisa cha Simba Aliyezama Kwenye Mapenzi

Hapo zamani za kale, Simba, mfalme wa mwitu, alitokea kumpenda binti mzuri wa jamaa mmoja mkata miti. Akapeleka maombi ya kinguvu ya kutaka amwoe. Baba wa binti yule, hakupenda kuruhusu mwanaye aposwe na mfalme Simba, lakini pia aliogopa kukataa ombi hilo.  Akajikuta...
Share:

Live Traffic Feed

Blogroll

BTemplates.com

Inaendeshwa na Blogger.

Jumla ya Mara Iliyotazamwa

Popular Posts