Tausi, kwa maringo na madaha aliupepeza mkia wake mpana na
kumdhihaki Korongo ambaye alikuwa akipita karibu yake, akimtazama kwa dharau kwa kuona rangi ya manyoya yake iliyofubaa na isiyovutia, akamwambia,
“Ona mimi nimevikwa joho la
kupendeza, kama mfalme vile, kwa rangi ya dhahabu na hudhurungi na rangi
nyingine zote za upinde wa mvua; ilhali wewe huna hata punje ya rangi ya
kuvutia kwenye mbawa zako.”
Tausi akimtambia Korongo |
“Ni kweli,” alijibu Korongo; “lakini mwenzio ninaruka na kupaa kwa
raha juu angani huku nikipaza sauti yangu kuelekea anga za mbali kwenye nyota, wakati wewe
unanatembea chini tu, kama jogoo, miongoni mwa ndege wala vinyesi.”
FUNDISHO; MANYOYA MAZURI HAYAFANYI NDEGE MZURI.