Mwanamfalme aliagiza Nyani kadhaa wapewe mafunzo maalum ya kucheza shoo. Kwa vile kwa asili Nyani ni waigaji wazuri sana wa matendo ya binadamu, walionyesha kuwa wanafunzi bora wenye kushika mafuzo haraka, na walipovishwa nguo na vinyago kichwani, walicheza vizuri sana hadi kulingana au kwazidi wacheza shoo binadamu.
Kwenye matamasha maonyesho yao mara nyingi yalishangiliwa kwa vifijo na nderemo, hadi siku moja jamaa fulani mcheza shoo mwenye wivu, aliyepania kuwafanyia hila, alitoa mfukoni mwake karanga za maganda na kuzirusha jukwaani.
Basi ikawa wale Nyani, baada ya kuona karanga wakasahau kazi yao ya kucheza na wakawa (na kweli walikuwa) Nyani badala ya Wachezashoo.
Walivua vinyago vyao na kuchanachana nguo walizovikwa, wakagombania karanga. Hivyo onyesho hilo likaishia hapo huku hadhira ikicheka na kudhihaki.
***